Latest News

Monday, January 27, 2020

Bikira za Kutengeneza Zaleta Mdahalo Mkubwa Uingereza



Wanawake wa Kiislamu wengi wanakuwa katika hatari ya kuuawa inapotokea wakathibitika kuwa wameolewa bila kuwa na Bikra. Baadhi yao wamejiwekea utaratibu wa kuwafuata madaktari ili kuwarudishia Bikra zao

Inagharimu hadi Paundi 3,000 sawa na Tsh. milioni 9, kwa upasuaji ambao huchukua takriban lisaa kukamilika. Wapiganiaji Haki za Wanawake wanasema, kliniki hizo zinafaidika kutokana na uwepo wa Waislamu ambao huogopa kuonekana sio wasafi siku ya ndoa

Kuna hatari ya kuwa kama utengenezaji wa Bikra utazuiwa basi kuna hatari kubwa ya waislamu kufanya hivyo kimagendo. Kuna takriban kliniki 22 ndani ya Uingereza ambazo zinafanya upasuaji wa kuweka tabaka la ngozi ili Mwanamke kurudi kuwa Bikra
-
Katibu wa Afya Matt Hancock amesema, wanachunguza namna ya kukomesha tukio hili ovu japo Idara ya Afya imekataa shauri hilo kutokana na ugumu wa kutekeleza zuio hilo

Wasichana wanaweza kuishia kufa kama kutakuwa na zuio la kutengeneza Bikra. Dkt. Khalid Khan, aliwahi shuhudia namna upasuaji huo unavyofanyika na kusema haitakuwa sahihi kuzuia upasuaji huo

No comments:

Post a Comment