Latest News

Saturday, April 1, 2017

ZIJUE KANUNI 30 KWAKO MWANAWAKE ULIE NDANI YA NDOA



KANUNI 30 KWA WANAWAKE NDANI YA NDOA

1). Usinyanyue sauti mbele ya mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima.

2). Usifichue udhaifu wa mumeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako. 

3). Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na mumeo, hujui namna mumeo atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.

4). Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.

5). Usiwatendee vibaya marafiki wa mumeo kwa sababu huwapendi, mtu anayetakiwa kuwa wa kwanza kujitenga nao ni mumeo.

6). Usisahau kuwa mumeo alikuoa, yeye si mfanyakazi wako au mtu mwingine tofauti. Tekeleza majukumu yako.

7). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mumeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mumeo ni jukumu lako mwenyewe.

8). Usimlaumu mumeo akija nyumbani mikono mitupu. Badala yake mpe nguvu, mhamasishe na kumshajiisha.

9). Usiwe mke mwenye matumizi ya hovyo, jasho la mumeo halitakiwi kutumiwa hovyo.

10). Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

11). Usimlinganishe mumeo na mwanaume wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.

12). Usijibishane na mumeo hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la mwanaume ni heshima.

13). Usimpe changamoto mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye busara hawafanyi hivyo.

14). Usisahau kumuandaa mumeo na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.

15). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.

16). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na kwenye dressing table. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao wanatumia muda wao kujiremba vizuri bila haraka yoyote ili waonekane maridhawa.

17). Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.

18). Usiegemeze upendo wako kwenye vitu vya pesa. Endelea kumheshimu mumeo licha ya kwamba unapata pesa zaidi yake.

19). Usisahau kuwa mume anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

20). Iwapo mawazo yako yamefanikisha jambo kuliko mawazo yake, usijilinganishe naye. Bali ishini na mfanye kazi kama timu.

21). Usiwe msumbufu kwa mumeo. Hakuna mume anayependa mke msumbufu.

22). Mke mvivu hajali. Hata hajui kwamba anatakiwa kuoga na kuwa msafi.

23). Je, mumeo anapenda chakula fulani? Kuwa makini sana kwenye namna ya utayarishaji wa chakula. Hakuna mume anayefanya maskhara na suala la chakula.

24). Usiwe mtu wa kumkamua sana mumeo, ukataka kila kitu uwe nacho wewe. Furahia kile kinachopatikana kulingana na uwezo wake.

25). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho wa kwanza kwa mumeo na kwa kila mgeni anayeingia nyumbani kwenu. Ukarimu maridhawa ndiyo uzuri wa kweli.

26). Usisuhubiane na wanawake wenye mtazamo hasi na wa kimakosa kuhusu ndoa.

27). Ndoa yako itakuwa na thamani kama utaipa thamani. Uzembe na kutojali ni sumu ya ndoa.

28). Watoto ni zawadi adhimu kutoka kwa Mungu, wapende na uwafunze mambo mazuri.

29). Umri usiwe kikwazo cha kuwa na ushawishi kwenye nyumba yako. Kamwe usipunguze kiwango cha huduma kwa familia yako kwa hali yoyote ile. Ifanye huduma yako kuwa yenye kujaa ubunifu maridhawa.

30). Mke anayemuabudu Mungu ni mke maridadi, daima muombee mumeo na familia yako.
Ninakutakia ndoa njema. Usisahau ku share na wenzako kusambaza ujumbe huu muhimu kwako na kwa wengine wapenda maendeleo...

No comments:

Post a Comment