Latest News

Friday, December 12, 2014

Exclussive; Kama ulikuwa haupata ule mkasa wa picha za utupu zilizovunja ndoa ya dokta hatimaye kupewa talaka..


Mwanamke ambaye pia ni DAKTARI wa Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja Zanzibar, Salha Hassan amejikuta akipigwa talaka na mume wake, Abdullatif Mohamed kufuatia picha zake chafu akiwa na mwanaume mwingine kunaswa kwenye simu yake mkononi, Uwazi limenyetishiwa. 
Cheti cha ndoa ya Salha Hassan na mume wake, Abdullatif Mohamed.
 Akizungumza kwa masikitiko makubwa, Abdul alisema alifunga ndoa na Salha Februari 15, 2007 na waliishi kwa upendo mkubwa.


Abdul alisema kuwa mwaka 2010 mkewe aliondoka Zanzibar na kwenda kuongeza ujuzi kwenye Chuo Kikuu cha Udaktari Muhimbili jijini Dar es Salaam.

“Akiwa pale Muhimbili mke wangu alinieleza kuwa simu yake ya mkononi (Nokia) inamsumbua sana, nikamshauri kwamba akirudi huku tuiuze halafu nimnunulie nyingine,” alisema Abdul. 
Aliongeza kuwa, katika mwaka wa tatu, mkewe alipofanya mtihani alifeli, hivyo akalazimika kurejea Zanzibar kuendelea na kazi katika hospitali anayofanyia kazi.


“Siku kadhaa baada ya kurejea, nilichukua simu yake kwa lengo la kwenda kuiuza kama tulivyokubaliana, lakini mke wangu alitoa ‘memory card’ yake ambayo najua mlikuwa na vikorokoro vyake, hilo sikulifuatilia. “Tayari nilishapata mteja, tukakubaliana bei lakini kabla ya kumkabidhi niliamua kufuta vitu vingine ambavyo vilikuwa ndani ya simu ya mke wangu. Wewe mwandishi unajua, simu zina ‘dokumenti’ mbalimbali,” alisema Abdul.

Abdul alisema kuwa akiwa katika zoezi la kufuta kumbukumbu mbalimbali zilizokuwemo kwenye simu hiyo, ghafla alizibamba picha chafu za mke wake akiwa na mwanaume mwingine ambaye hakumjua. “Nilishtuka sana, sikuwahi kufikiria. Hata hivyo, awali nilidhani naota ndoto, lakini baadaye nikajiridhisha kwamba sikuwa ndotoni,” alisema Abdul.


Mwanaume huyo aliongeza kwamba, kufuatia tukio hilo baya machoni mwake alijikuta akianguka na kupoteza fahamu.

Abdul alimuonesha paparazi wetu picha alizozinasa ambapo moja, Salha anaonekana amelala kitandani akiwa amenyoosha miguu kwa kujisitiri na ‘kufuli’ tu. Picha nyingine amepozi kwa kuegemeana na mwanaume huyo ambaye Abdul alisema anaamini anaishi jijini Dar es Salaam au alikuwa akisoma naye Muhimbili. Picha nyingine, Salha anaonekana amepozi katika mkao tata akiwa mtupu. Picha mbili zilionesha alijipiga mwenyewe isipokuwa ile aliyolala kitandani.

Abdul alisema kuwa kufuatia kuuona uozo huo wa mke wake aliyempenda sana, baada ya kuzinduka alibatilisha uamuzi wa kuiuza simu hiyo na kurejea nyumbani ambapo alipomuuliza, mwanamke huyo hakuwa na majibu ya kujitosheleza. Waligombana sana na mwishowe aliamua kumrudisha nyumbani kwa wazazi wake ‘akimsindikizia’ talaka juu kwamba si mke wake tena.

Akasema: “Kwa kweli sikuweza kukivumilia kitendo kile, haikuwa nia yangu kumpa talaka lakini moyo ulishindwa kuvumilia kuona mke wangu yupo kama alivyozaliwa.

Baada ya kuzinyaka habari hizo, gazeti hili lilimtafuta Salha kwa njia ya simu yake ya kiganjani ambapo baada ya kumpata na kumsomea mashitaka yake kuhusu picha hizo, alijibu kwa jeuri: “Mimi naona ulizokuwa nazo (picha) hazikutoshi kabisa. Ninazo nyingine, kama upo tayari nikutumie ili uziongezee kwenye habari yako. Kwanza mimi siyo daktari. Uwazi: Sikia Salha… Salha akakata simu.

Uzoefu unaonesha kuwa, tangu simu za mkononi zilipoingia nchini Tanzania, wapendanao, wakiwemo wachumba, wamekuwa wakiingia kwenye migogoro mikubwa inayosababishwa na matumizi mabaya ya simu hizo. Ni vyema wapendanao wakachukua tahadhari kuhusu matumizi ya simu zao. Baadhi ya wafuatiliaji wa masuala ya ndoa wanasema kuwa hakuna kiwango cha juu cha wanandoa kutopendana kama usaliti..

No comments:

Post a Comment