Mwanamume wa kwanza duniani kushika mimba ashtakiwa kwa kumfuatilia mke wake kupitia kifaa cha GPS kilichobandikwa kwenye gari ya bibi huyo.
Thomas Beatie alizaliwa mwanamke lakini baadaye alijibadilisha jinsia na ‘kuwa’ mwanamume. ‘Jamaa’ huyu ana tupu zote mbili. Thomas Beatie alifunga ndoa na mkewe Nancy Beatie mwaka 2003 na kujifunguwa mwaka 2008 baada ya kujipachika mimba kupitia maabara (artificial insemination). Thomas aliamua kubeba uja uzito kutokana na hali tasa ya mkewe.
Jamaa huyo mwenye miaka 40 anadaiwa kumfuatilia mtalaka wake kwa kutumia kifaa cha GPS, jambo lililopelekea kutiwa kwake mbaroni.
Mtu mmoja ambaye ni mfanyikazi wa serikali, alikigunduwa kifaa hicho kwenye gari la Bi. Beatie alipokuwa anamsaidia kubadilisha gurudumu lililopata panchari mjini Phoenix, Arizona.
Ingawa Thomas Beatie ameshtumiwa kwa kumfuatilia mtalaka wake, bado ni mshukiwa tu na anatarajiwa kufika mbele ya koti kujibu mashtaka.
Katika mahojiano na polisi, Thomas alikiri kukitipachika kifaa hicho kwenye gari la Nancy mwaka 2012 wakati gari hilo lilipokuwa chini ya miliki yake. Kifaa chadaiwa kuwashwa miezi sita baada ya Thomas kumpa Nancy makaratasi ya talaka. Wakati huo, koti ilikuwa imetoa amri ya kumlinda Thomas dhidi ya Nancy kwa kuwa alijaribu kumvamia.
Bi. Beatie alielezea polisi kwamba alikuwa akishangaa ni vipi alikuwa akikumbana na mtalaka wake ghafulamara kwa mara katika sehemu tofauti huku akitaka kujuwa alikuwa ametoka wapi na anaenda wapi.
Mnamo mwaka 2007, Bwana na Bi. Beatie walinunua manii kutoka kwa mtu kupitia mtandao ambayo yaliyopachikwa ndani ya Thomas na baadaye kujifungua mtoto wa kike mwaka 2008 waliemuita Susan. Thomas alizaa tena watoto wawili baadaye.
Licha ya panda shuka walizopitia kama wanandoa, waliachana baada ya Thomas kutaka talaka na kupewa dhima ya watoto mnamo Mei 2012.
Iwapo Thomas Beatie atahukumiwa na kosa la kumfuatilia mtalaka wake, wadadisi wasema si rahisi kwamba atapewa kifungo bali huenda akapewa onyo na mahakama ikiangaziwa ni kosa lake la kwanza.
No comments:
Post a Comment