Wiki iliyopita tulieleza kwa urefu kuhusu tatizo la fangasi kwa wajawazito baada ya kueleza tatizo la kuwashwa sehemu za siri kunakotokana na fangasi na tukaahidi kwamba tiba na ushauri tutafafanua leo.
Kabla ya kueleza tiba tufafanue kwamba kuna baadhi ya mambo yanayosababisha watu kuwashwa sehemu hizo nyeti kama vile kuwa na fangasi tuliowataja katika matoleo yetu yaliyopita.
Wengine huwashwa kutokana na kutumia dawa za antibayotiki kwa muda mrefu. Dawa za antibayotiki ni kama, ampicillini, amoxyclini, ciproflaxine, doxylline, erythromycine, gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa hizi bila ushauri wa daktari.
Kutumia dawa hizo husababisha fangasi kwani huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha sehemu za siri kukiwa hakuna kinga. Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwa sababu unene husababisha jasho sehemu za siri na kuongeza unyevunyevu sehemu hizo, pia michubuko kutokana na kubanwa na chupi.
Sababu nyingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama prednisoline, hydrocortisone, dexameltasone na nyingine nyingi. Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi sehemu nyeti.
Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi.
Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.
Dalili
Dalili kwa maradhi ya fangasi hutofautiana kati ya mtu na mtu ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho sehemu za ndani au kwenye mashavu ya sehemu za nje za siri za mwanamke.
Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara.
VIPIMO
Wote wenye dalili hizo wanashauriwa kwenda kwa daktari ambapo baada ya kumuona ataanza kumchunguza mgonjwa sehemu yake ya siri ambao kitaalamu huitwa PV exam.
Daktari pia atachunguza kama kuna uchafu wowote unaotoka, wingi wake, rangi yake, harufu yake, na mgonjwa awe huru kumsimulia daktari tatizo lake kama anaona haya niliyoyataja.
Mgonjwa atachunguzwa kama ana mitoki sehemu za siri na daktari ataangalia shingo ya kizazi, sehemu ya haja kubwa kama kuna bawasiri (haemorrhoids) nk.
No comments:
Post a Comment