MSANII anayechipukia kwa kasi katika anga la filamu Bongo, Sabrina Omary ‘Sabby
Angel’ amefunguka kuwa kwa kipindi kifupi ambacho amezama kwenye penzi la staa wa Bongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior’, amempa mahaba mazito kiasi cha kumfanya asimkumbuke aliyekuwa mkewe.
Akizungumza na mwanahabari wetu, Sabby alisema kuwa ameamua kuonyesha ufundi wake wote wa kimahabati kwa msanii huyo kwani ni mwanaume ambaye amemuona mwenye mapenzi ya dhati.
“Sijawahi kukutana na mwanaume mwenye mapenzi kama huyu na mimi zawadi nitakayompa ni mapenzi mazito na nitamaliza ufundi wangu wote kwake na kamwe hatokumbuka kama aliwahi kuwa na mke kabla yangu,” alisema Sabby.Bob Junior aliwahi kumuoa mwigizaji, Halima Ally kisha wakamwagana baada ya kuzaa naye mtoto mmoja.
No comments:
Post a Comment