Latest News

Mapenzi

Habari

Laana

Umbea

Recent Posts

Friday, July 19, 2024

EX WA ASAKE ATOA SIRI YA MAFANIKIO

 


 Ex Girlfriend wa Msanii Asake ( i.e Madam Mystiquee 🦋) alivyoweka wazi sababu ya kishetani ( i.e freemason) iliyopelekea mahusiano yao kuvunjika.

Wawili hao waliachana ghafla ,wengi hawakujua chanzo mpaka pale mmoja wa mashabiki wa Asake alimuuliza kwenye comments katika ukurasa wake wa Instagram


Akisema "Why did you break our national sweetheart's Our Asake "


Yeye akiandika "cuz he wanted to go let the devil use him.."


Sababu io ikapelekea kuzua gumzo, na wengi wakiwaza kuhusu Asake kujiunga na freemason, jambo ambalo halikutambulika awali na wengi hususani mashabiki zake likiwekwa wazi na aliyekuwa Ex wake Hit maker uyo wa Amapiano ..

Sunday, September 13, 2020

TAMBUA JINSI YA KUONGEZA MVUTO KWA MPENZI WAKO.

 


Mwenzako alikuwa ameshafikiria suala la kuingia kwenye ndoa na wewe lakini kwa sababu ameshakushusha thamani ndoa inaweza kuyeyuka.


Ukiwa kwenye ndoa ni hatari zaidi maana mwenzako hukuchukulia wa kawaida – mazoea huzidi na hapo ndipo uhitaji wa kuwa na mwingine wa pembeni unapoanzia. Haoni cha muhimu tena kwako, ndiyo maana wazo hilo huvamia ubongo wake kwa kasi sana.

Itafikia hatua, kama upo ndani ya ndoa, mwenzako atagoma kuongozana na wewe na kama ikitokea hivyo mkikutana na rafiki zake njiani hatakutambulisha. Hisia kwamba hamuendani humwingia.


UNAFANYAJE SASA?
Kubwa unalotakiwa kufahamu rafiki yangu mpendwa, suala la kupanda au kushuka thamani lipo mikononi mwako. Yapo mambo ambayo ukiyazingatia, mwenzako hawezi kukuchoka na kufikia hatua ya kukushusha thamani.
Tayari tumeshaona athari zake lakini hapa sasa nataka kukupa mbinu ambazo ukiwa nazo makini basi itakuwa rahisi kwako kubaki namba moja na mtu muhimu zaidi (ndiyo inavyotakiwa kuwa) kwa mpenzi wako maana ni haki yako.

ANZIA MWANZO
Ni rahisi zaidi kulinda thamani yako kuanzia mwanzo wa uhusiano wenu. Ikiwa tayari mmeshakomaa halafu tatizo hilo likajitokeza, hutumika nguvu nyingi zaidi kulirekebisha kuliko kujizatiti kuanzia mwanzo wa uhusiano. Ni mambo gani hayo? Twende hapo chini.

CHUNGA KAULI ZAKO
Naomba ieleweke wazi kuwa mada hii ni maalum zaidi kwa wanawake. Kitu muhimu cha kwanza kabisa kwa mwanamke ambaye anataka kuilinda thamani yake kwa mpenziwe ni kupima sana kauli zake.
Acha kuropoka hovyo, pima maneno yako na ikiwezekana kama unadhani kuna jambo huna uhakika nalo usizungumze kabisa. Katika eneo hili, uwe makini zaidi mnapokuwa na watu wengine. Kama mwanamke usiwe mchangiaji hoja sana.
Utulivu wako unaweza kuwa silaha kubwa ya kukufanya ubaki na thamani yako kama mwanamke anayejitambua.

USIRUHUSU MAPENZI

Msichana mwenye kujitambua na kufahamu thamani yake sawasawa hawezi kuruhusu mwili wake ujulikane na mwanaume harakaharaka. Onesha unajitambua na usikubali kirahisi kuuacha mwili wako uchezewe.
Mpe hoja; kwanza mapema, hajakuoa wala kukuchumbia, haraka ya nini? Wakati unawaza kuhusu kutoa penzi lako, lazima ufikirie kuhusu athari zinazoweza kukupata kwa kukurupukia mapenzi. Mwanaume ambaye bado hamjachunguzana na huna uhakika naye wa kutengeneza maisha, kichwani mwake hakuweki kwa asilimia kubwa.

Thursday, January 30, 2020

Amenisomesha, Kaninunulia Gari Lakini Sina Mapenzi Naye! Nifanyeje?


Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28 Naishi Tabata jijini Dar nimejitokeza kwenu kuomba ushauri, Mimi na mpenzi wangu ambae amenisomesha toka form one hadi sasa nipo chuo kwani wazazi wangu walifariki wakati mimi nikiwa mtoto mdogo sana.

Sasa huyu mpenzi wangu amenigharamia sana yani kuanzia nguo zote hadi chakula nacho kula vyote ni msaada wake yeye na amejitolea kuninunulia gari la kutembelea na kanambia nitafute kiwanja ili tujenge nyumba ya kupangisha.

Ila mimi kwa sasa naona kama huyu mwanaume hatuendani kwani yeye hana elimu ila anafanya kazi kutumia akili ya kuzaliwa, Jamani mimi nataka kuishi na msomi mwenzangu ila huyu kaka mimi naona kama freemasson kwani kanisaidia sana asije akanitoa kafala, Mimi kwa sasa nimepata mpenzi mpya ambae anaelimu ya chuo pia ni sharo sio mshamba kama huyu wa zamani.

Sasa please naombeni ushauri wenu jamani nimwambiaje kama sipo tayari kuishi na yeye huyu mpenzi wa zamani bila kuumiza moyo wake...?

Rose Ndauka Aeleza Alivyotumika Kwenye Maisha yake


Msanii wa filamu Rose Ndauka, amefunguka na kusema kipindi ambacho ametumika sana kwenye maisha yake ni pale alipokuwa kwenye umri wa ujana na ujinga "Foolish Age" ambapo alikuwa anapenda starehe kupitiliza.



Rose Ndauka amesema katika umri huo wa kijinga, ametumika sana kwa kwenda kwenye kumbi za starehe kuanzia Ijumaa hadi Jumapili.


"Muda ambao nahisi nimetumika ni ule wakati nakuwa na umri wa kijinga na ujana "Foolish Age" maana nilikuwa naenda club kuanzia Alhamisi hadi Jumapili, tena ilikuwa ni sababu ya marafiki ambao wamenizunguka ila nashukuru Mungu nimebadilika, sasa hivi naishi kwenye ndoto za maisha yangu" amesema Rose Ndauka.

Aidha Rose Ndauka amewachana wanawake ambao wanategemea kudanga ili kupata pesa kwenye maisha yao kwa kusema.


"Unaweza ukawa na sponsor "danga" kibao, lakini ukaishia kupiga picha za selfie hotelini, kula na kununua nywele lakini hautafanya kitu cha maana, ila mimi nimepambana mwenyewe hadi kufikia hapa kufungua ofisi yangu na kuajiri vijana wengine"

Rose Ndauka kwa sasa ni Mkurugenzi katika ofisi yake inayojishughulisha na masuala ya urembo.

Wednesday, January 29, 2020

Ukiamua Kuwa na Mahusiano na Mume wa Mtu Lazima Ukubali Kuwa Mtumwa wa Mambo Yafuatayo



Ukiamua Kuwa na Mahusiano na Mume wa Mtu Lazima Ukubali Kuwa Mtumwa wa Mambo Yafuatayo:
1. Baby samahani dakika moja,wife anapiga simu

2. Baby muda umeenda Sana mke wangu atanipigia, wacha niwahi kurudi nyumbani, Kesho saa 12 nitakuwa hapa

3. Bby nataka kuja kulala kwako mke Wangu amefiwa kaenda kwao

4. Baby sintaweza kuja Leo, wife kanibana... Pole kwa kuugua

5. Baby tangulia mbele, nitakukuta... Pale wanakaa shemeji zangu, wakituona pamoja watamuambia wife

6. Unaweza kimbiwa katikati ya sherehe usipewe hata nauli ya bodaboda, kesho unaambiwa sorry darling, si uliona wife alitokea ghafa

7. Mkiwa mnaongea kwa simu kwa mahaba mara unashtukia unaitwa Hamadi na kuagwa fasta.,baadae unaambiwa mke wangu alitokea ghafla nikawa sina jinsi

8. Unaweza pitwa barabarani na mvua inanyesha,kesho ukaambiwa nilikuona my love, Ila ningefanya nini.. ,nilikua na mke wangu

Ili mwisho wa siku ukija kupewa mimba na kuterekezwa usije na kauli zako za kusema wanaume wote ni mbwa😂😂na kama utafikia hatua ya kuwaita wanaume wote hivyo basi anza na kumtaja baba yako ili twende sawa maana sometimes huwa mnakuwaga na ukulunjuma mwingi sana dadeq
Music