Yere…yere masela inakuwa nini pale kati? Kwani kuna problemu? Kitaa hii ni mpeto wanangu hakuna kusebenza kozi hapa vumbi tu. Ukifuata nyayo tunatembea na fagio tunazifuta. Kitaa hiyo kwa fasi ya Roki Siti barida? Kama vipi mzuka tu makiksi wangu.
Wanangu deizi zinakrosi kama hazina akili flenga na watu wazima bado mambo siyo freshi kozi hatujamaliza kurekebisha ishu f’lani za mkwanja ili kitu cha eksimasi kiende levo. Dah! Mazee ukisikia kuchekwa si ndo kama hivi? Wana na marelativu ujue wanasikilizia tu mwana nirekebishe dheni kitu cha holidei kieleweke. Wangejua tu nipo apeche alolo wangeminya kimtindo kama vile hawanioni bati ndo kwanza pipo zimekomaa si unajua zile mimi ndo taita wao? Kama vipi kaa humu wewe uinjoi.
Juzikati bana, nilikuwa kwenye msele kitaa cha Kinokleini. Huku na huku nikaona nizame hapo kwa fasi ya Feisibuku nini nigonge angalau kitu cha kiepe na juisi ya ukwaju. Taimu ikafika mzigo ukatimba kwa tebo dheni mtu mzima nikaanza kupeleka pwani.
Wakati napiga vitu vyangu, shaaa…mwanangu Dick naye akawa anapaki ule mkoko wake uliochoka kidizaini utadhani alipewa nyongeza. Hivi makachaa mnajua kuna ndinga mkienda kubai mnapewa nyongeza? Huku tauni wana wanaita kiini cha yai…tehee… eti tauni hakuna faza mwenye ndinga bati kuna faza mwenye hausi. Hivi ni kweli wanangu? Oya kama nimekutachi usimaindi si unajua haya ni mastori ya wana ya kitaa?
Basi bana, mnyama wangu Dick anaonekana hayupo hepi kabisa aisee arifu!
Oya kachaa inakuwaje mbona mambo ya kubonyea kwa sana? Nilimsabahi kibishi selaa dheni nikamwambia anijoini tupige kitu cha kiepe na madikodiko kibwena.
Chezea kitu cha firigisi pale kati?
Basi bana…msela wangu kaniteli kuwa lasti yia alimiiti na shori mmoko mkare aibu. Bati truli ni kwamba yule mtoto Dick hakumlavu ileile isipokuwa alimtamani tu kozi shori ana hoja tena hoja nzito kinoma.
Mzee mnyama mwenyewe Dick akategemea kuwa akimsarendea atavuliwa kitu cha kufuli fasta ainjoi mambo f’lani? Aah wapi shori akamteli kuwa ataweiti kinoma.
Mshkaji alichowaza wala shori hakuwa na aidia nacho. Jamaa akawa anamfanyia shori taimingi ili ale mambo dheni atambae. Nani kakudanganya inaweza kuwa simpo kiasi hicho? Jamaa yangu akaona gia freshi na kumuwini mtoto mzuri ni kumpromisi kwamba atamgonga kitu cha mereji. Kweli bana msela anakuteli kuwa taimu iliposonga shori akawa kama vile amemwelewa.
Mwana kuona hivyo akaongeza spidi hadi yule mtoto mzuri yaani sumu hasa akawa amezima fegi kwa kachaa. Jamaa anakuminya kuwa kuna taimu alikuwa anajifanya yupo siki dheni shori anahangaika hadi anampiga mzinga mshua wake kozi ni mambo safi ili tu ampelekee jamaa akatibiwe.
Kwa kuwa shori alimpromisi msela kila kitu isipokuwa mambo ya siksi bai siksi, mwanangu akawa anavuta mkwanja dheni anaenda kutumbua na maduu na vichenchede wa fasi ya tauni. Chezea watoto wa tauni weye? Ukikaa vibaya unauza hata nyumba ya urithi daadeki!
Ebana siku moko msela amepiga vitu vyake hadi akawa njwiii…akamuibukia shori. Alipotimba kwa geto la shori, jamaa akawa anataka mambo f’lani kwa nguvu!
Alipoona mrembo hamsomi akaona isiwe kitu, akaamua kumlewesha na mambo meupe kisha akajipigia mzigo kama anavyomaindi.
Zilipita siku bee dheni shori akamuibukia mwanangu kisha akamfungukia ishu nzima kwamba yeye ni mwathirika wa ngoma kitambo na dei aliyomrukia dheni aliukwaa. Acha mwanangu atokwe na macho utadhani mjusi kabanwa na mlango. Mtoto mzuri akamwambia kwa kuwa alimvaa bila kinga ni beta akaenda kucheki ili aishi kwa mahopu.
Kweli msela amepima kitu kipo positivu so amechanganyikiwa kinoma. Yaani bata la dei moko likawa limemkosti laifu lote lililobaki. Hiyo yote ni kwa sababu ya kurukaruka wanangu. Masela tulieni, mambo ya kurukaruka tuachieni popkoni.
Kwa info yako kama huwezi kutulia shauri yako kozi ripoti karenti zinaonesha kwamba wana wengi hawatumii kitu cha kinga so maambuki yameongezeka twaisi aise! Jilinde!
Mmenisoma masela? Kama vipi sii yuu neksti wiki!

No comments:
Post a Comment