Latest News

Friday, November 14, 2014

MADENTI MNAJILINDA, SISI MAANKO NI MAFISI!


Mambo aje maanko? Poleni sana kwa wale wa kidato cha nne ambao mmetoka kumaliza
mitihani yenu, mnasikilizia matokeo hapo mwakani kama vipi, wale waliofanya vizuri waendelee na elimu ya juu zaidi. Nina uhakika wengi watafaulu kwa sababu walitumia muda wao mwingi katika kuhakikisha wanapiga kitabu kama hawana akili nzuri, enzi zetu tuliwaita akina John Kisomo!
Tunakumbuka mara ya mwisho tulivyowasiliana, tulizungumza kuhusu mambo hayahaya ya mitihani, nikawaambia kuwa huu ndiyo mwanzo wa safari ndefu ya maisha. Kwamba kidato cha nne, ndiyo sehemu ambayo maisha yanaanza, kwa sababu tayari unakuwa umeshapevuka kiakili na angalau unafahamu nini maana ya maisha!
Leo ninataka kuzungumza na maanko zangu wa kike, kwa sababu wao ndiyo waathirika wakubwa wa maangamizo ya kimaisha. Wakiwa shule na hata baada ya kumaliza kidato cha nne, wanakuwa na majaribu mengi, yote kutoka kwa wanaume wanaowataka kimapenzi.
Ninakumbuka sana, wakati ule tukiwa shule, kulikuwa na wadada walikuwa wazuri sana wa umbo na sura, mabitozi wa mjini walikuwa wanapishana kila siku kuwagombea. Wenye hela ndiyo walikuwa wanawachukua kirahisi, si unajua maisha ya shule na tamaa za wadada?
Na ukumbuke, hawakuwa mabitozi na wenye fedha tu waliokuwa wakiwakimbiza dada zetu enzi hizo, bali hata walimu nao walikuwa wakigongana kwa wanafunzi. Ninakumbuka huko nyuma nilishawahi kuwasimulia juu ya kisa cha ticha mmoja hivi, ambaye alikuwa rafiki yetu. Aligombana na mmoja wa washkaji kwa sababu ya kutaka kumtisha na kumchukua demu wake.
Kifupi ni kwamba wasichana wa shule, hasa sekondari na vyuo, wanakuwa katika kipindi chao cha hatari zaidi katika maisha yao kuliko wakati mwingine wowote. Hii ni kwa sababu wanakuwa ndiyo kwanza wanachanua, kama maua yanavyotokeza katika mimea mbalimbali.
Katika kipindi chao cha kuchanua, kila mmoja huonekana mzuri mbele ya macho ya wanaume. Na kumbuka, hapa ninazungumzia wanaume, bila kujali kama ni vijana wenzao au watu wazima. Niwadokezee kidogo, wanaume wanapenda sana dogodogo na wapo tayari kwa lolote. Lakini bahati mbaya sana, wasichana wa shule, siyo watu wa kutaka mambo makubwa, wanaishia kupewa hela ya chips kuku.
Na kwa sababu ya tamaa zao, hujikuta wakishiriki mapenzi. Kwa kuwa hata katika eneo hili nako wanakuwa bado ni wanafunzi, wengi wao hujikuta wakifanya bila kujilinda. Matokeo yake, wanapata magonjwa au mimba. Vyote ni hatari.
Ninataka kusema nao kwa sababu mimi ni mzazi wa kisasa, sitaki kuwa kama wazazi wangu ambao hawakumwambia dada yangu juu ya mambo haya. Walimwambia kwa mafumbo ya kiutu uzima ambayo alipokuja kuyaelewa, tayari alikuwa ameshachelewa!
Hakuna wakati muhimu katika maisha ya msichana kama ujana. Hapa ndipo unapoweza kujenga au kubomoa future yako. Tunashuhudia, wengi wanapata mimba au magonjwa katika wakati huu kiasi kwamba wakati mwingine unatikisa kichwa na kujiuliza inakuwaje binti huyu wa miaka chini ya 18 eti ana ukimwi!
Ni wakati wa vishawishi vingi, vyote vikilenga kukurubuni ili uwahi kuingia katika ulimwengu wa mapenzi, ambao kiukweli, hauwezi kukusaidia zaidi ya kukuharibia. Ukipata mimba, unajidanganya kwamba utatoa, sawa utatoa, lakini unajua kutoa mimba ni dhambi na vilevile ni kosa kisheria?
Utatoa ya kwanza, ya pili au hata ya tatu. Habari mbaya ni kwamba wanaotoa mimba sana ujanani, wanajutia ukubwani kwani we


No comments:

Post a Comment